Monday 21 November 2016

#YALIYOJIRI>>>Rais Magufuli akutana na kiongozi wa Jeshi la Ukombozi la China.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 21 Novemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong, Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Viongozi hao wamezungumzia uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na China katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika masuala ya ulinzi ambapo Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) limekuwa na ushirikiano na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA)
 
Rais Magufuli amemueleza Jenerali Fan Changlong kuwa Tanzania inathamini ushirikiano huo ambao umechangia kufanikisha juhudi za kuimarisha JWTZ zinazolenga kuwa na Jeshi la Kisasa na vifaa bora.
 
Dkt. Magufuli amemuomba Jenerali Fan Changlong afikishe salamu na shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika kuimarisha majeshi ya ulinzi na pia katika masuala mengine ya maendeleo ya kijamii.
 
“Nimefurahishwa na ziara yako hapa nchini kwetu, ujio wako unazidi kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zetu ulioasisiwa na waasisi wa mataifa haya Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Hayati Mwenyekiti Mao Tse-tung wa China.
 
“Naomba unipelekee salamu zangu kwa Rais Xi Jinping na umwambie kuwa pamoja na kuendeleza uhusiano na ushirikiano wetu katika kuimarisha majeshi pia tunatarajia kuona China inakuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi zetu za maendeleo kwa kujenga viwanda na kushiriki katika miradi mingine ukiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard Gauge” amesema Rais Magufuli.
 
Kwa upande wake Jenerali Fan Changlong amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi imara aliouonesha katika Awamu ya Tano na amemhakikishia kuwa China itaendeleza na kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania katika masuala ya usalama hasa kuimarisha JWTZ.
 
Jenerali Fan Changlong amesema Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China na Jeshi la Wananchi Tanzania yana uhusiano wenye manufaa makubwa na kwamba hivi sasa yanafanya uboreshaji utakaoyaimarisha zaidi na kuwa majeshi ya kisasa.
 
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Makamanda wa Majeshi wa Tanzania na China.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwa mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong wakati wakelekea kwenye ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wake akiongoza mazungumzo rasmi na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Watu wa China(PLA) pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
21 Novemba, 2016

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

0 comments:

Post a Comment