Thursday 21 September 2017

Madaktari Nchini Kenya Washangaa Tundu Lissu Kuwa Hai.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema madakatari nchini Kenya wameshangazwa kumwona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa hai kutokana na shambulio la risasi lililotokea Septemba 2017 mjini Dodoma.

Msigwa aliyekuwa miongoni mwa viongozi wa Chadema waliomsafirisha Lissu kutoka Dodoma siku hiyo kwenda jijini Nairobi, aliliambia gazeti hili jana kwamba Lissu alivuja damu nyingi na kama asingepata huduma ya haraka angefariki.

“Tulipofika Nairobi, madaktari walishangaa kuona Lissu akiwa hai, kwa sababu alipoteza damu nyingi sana. Lakini niwashukuru sana madaktari wa hospitali ya Dodoma General kwa huduma waliyotoa kufanya Lissu tufike Nairobi,” amesema Mchungaji Msigwa na kuongeza:

“Nataka tu niwaambie Watanzania kwamba Tundu Lissu wetu aliumizwa sana katika jaribio la kuchukua uhai wake. Watu wasichukulie kama ni jambo dogo, ni jambo kubwa lililoharibu hata akili za watu tuliokuwa karibu naye.”
TOA MAONI YAKO

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment