Friday 29 September 2017

Ujumbe wa Ancelotti Baada ya Kufukuzwa.

Baada ya kufutwa kazi aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti ameishukuru bodi ya timu hiyo kwa kumwamini pamoja na ushirikiano waliompa katika kipindi chote alichofundisha timu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ancelotti ameandika “Imekuwa heshima kubwa kuwa sehemu ya historia ya Bayern Munich. Napenda kuishukuru Klabu, Wachezaji na zaidi mashabiki wa kushangaza ambao sijawahi kukutana nao tangu nianze kufundisha soka”.
Mtalaam huyo wa ufundi mwenye miaka 58 alipoteza kibarua chake jana mchana baada ya bodi ya Bayern Munich kuketi na kocha huyo na kuazimia kutoendelea na mkataba wake uliokuwa unamalizika 2019.
Baadhi ya wachezaji wa Bayern Munich Thiago Alcantala, Frank Ribery, Robert Lewandowski na Arturo Vidal wamemshukuru Ancelotti kila mmoja akieleza kwa namna ambavyo amefaidika kuwa chini ya kocha huyo kwa msimu mmoja


Tupe Maoni Yako

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment