Thursday 28 September 2017

Muziki wa Ali Kiba ni Mzuri Zaidi ya wa Diamond- Faiza.

Muigizaji wa Filamu Bongo, Faiza Ally amefunguka kuupa zaidi muziki wa Alikiba kuliko ule wa Diamond.
Faiza amesema hayo katika mahojihano na TBC Fm kwa kueleza kuwa Diamond ni mburudishaji wa jumla aliyeleta mapinduzi ya kimuziki lakini Alikiba muziki wake ni bora zaidi.

“Kwanza kati ya muziki wa Diamond na Alikiba, naupenda sana muziki wa Kiba, muziki wake ni mzuri kuliko wa Diamond,” amesema Faiza na kuendelea.

“Diamond ni ile full Entertainment ukimwalia tu unatabasamu lakini Kiba ana muziki mzuri. Nikizungumzia mtu aliyeutoa muziki akaupa heshima mpaka akampa changamoto Kiba na yeye akasimama mpaka tukaanza kumuona kwenye hali ya tofauti ni Diamond,” amesema.

Ikumbukwe kuwa September 3 mwaka huu Faiza aliandika ujumbe katika mtandao wa Instagram na kueleza  kuwa kumpenda Diamond ni jambo la lazima na sio ombi kutokana na mengi mazuri aliyofayanya katika muziki wa Bongo Flava.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment