Monday 18 September 2017

MAHAKAMA: Upelelezi wa Awali Kesi ya Aveva na Kaburu Umekamilika.

Upelelezi wa awali katika kesi ya utakatishaji fesha inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa leo September 18, 2017 kuwa, upelelezi wa awali wa kesi hiyo umekamilika ambapo jalada la kesi limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili alisome na kueleza kama anaona umekamilika au la.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi September 27, 2017
TOA MAONI YAKO

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment