Thursday 21 September 2017

Mbao FC Imeahidi Kuichakaza Simba na Kubeba Pointi 3 Leo.

Klabu ya Mbao FC kutoka jijini Mwanza imeahidi leo kuchukua ushindi dhidi ya Simba na kubeba pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaochezwa leo katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mbao FC ambao wao ni wenyeji wa mchezo wamejigamba kushinda mchezo huo kwa kutumia nafasi ya wenyeji wao kuigalagaza klabu ya Simba ambayo nayo imetinga jijini Mwanza toka mwanzoni mwa wiki kujiandaa dhidi ya Mbao FC.

"Siku ndio leo vijana wenu tunajitupa Uwanjani kuumana na Simba kwenye Ligi Kuu ya Vodacom. Jitokezeni kwa wingi CCM Kirumba kutupa hamasa vijana wenu ili kuhakikisha mnyama anakaa mapema. Mechi itakuwa ngumu lakini sisi ndio wenyeji kwa hiyo tuna kila sababu ya kushinda maana mcheza kwao hutunzwa" Imesema taarifa ya Mbao FC

Klabu ya Mbao FC ni kati ya klabu ambayo iliipa shida Simba msimu uliopita katika mechi walizokutana ambapo Simba alishinda mechi hizo lakini ni kwa shida sana.

TOA MAONI YAKO

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment