Friday 29 September 2017

Mwanaume Aliyeshauriwa na Mganga Kufanya Mapenzi na Punda Atupwa Jela.

Mwanamme mmoja nchini Afrika Kusini aliyetambulika kwa jina la Ntando Mankungwini ametupwa jela mwaka mmoja baada ya kukutwa akifanya mapenzi na Punda.

Ntando (23) alikutwa usiku wa Jumatano ya septemba 20 mwaka huu kwenye zizi la nyumba jirani na nyumbani kwao mjini Mount Fletcher, Afrika Kusini akiwa nyuma ya punda usiku wa manane, kitendo ambacho wamiliki wa punda huyo walijua kuwa ni mwizi ila walikuja kustuka baada ya kumlika tochi na kumkuta akiwa utupu.

Wamiliki hao wa punda walimkamata na kumpeleka polisi na ndipo mtuhumiwa alikutwa na makosa ya unyanyasaji wa wanyama.

Mtuhumiwa akiwa Mahakamani alikiri kosa hilo la kufanya mapenzi na punda huyo huku akieleza kuwa alitekeleza sharti alilopewa na mganga wa kienyeji.

Ntando amesema alienda kwa Mganga wa Kienyeji kusaka dawa ya kuongeza nguvu za kiume na ukakamavu, ndipo aliposhauriwa kutembea na Punda.

Tayari mahakama ya mwanzo wilayani Mount Fletcher, Cape Town imetoa hukumu jana kwa kumfunga mwaka mmoja jela kwa kosa la unyanyasaji wa wanyama.




Tupe Maoni Yako

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment