Thursday 28 September 2017

Uganda Yafuata Nyayo za Tanzania Yapiga Stop Bunge Kuonyeshwa Live.

Vyombo vya habari nchini Uganda vimezuiwa kuonyesha moja kwa moja matangazo ya Bunge ambalo linaendelea na vikao.

Mkurugenzi wa Tume ya Utangazaji nchini humo, Godfrey Mutabuzi amesema redio na runinga zote haziruhusiwi kurusha matangazo ya Bunge moja kwa moja kuanzia leo Alhamisi.

Amesema sababu ya Bunge kutoonyeshwa moja kwa moja ni za kiusalama.

Wabunge nchini Uganda walipigana jana Jumatano ndani ya ukumbi wa Bunge wakiwa katika siku ya pili ya kikao cha kujadili muswada wa kuondoa ukomo wa miaka ya kugombea nafasi ya Urais kwa mujibu wa Katiba ya Taifa hilo.

Katika ugomvi huo, wabunge walirushiana viti na kuharibu vipaza sauti. Kikao hicho kiliongozwa na Spika wa Bunge, Rebecca Kadaga.

Ugomvi huo ulianza pale Spika alipochukua hatua ya kuwafukuza wabunge wapatao 25, wengi wao wakiwa ni wa upinzani kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Mwingine aliyetolewa ndani ya ukumbi ni waziri wa Serikali aliyeshtakiwa kwa kufyatua risasi bungeni Jumanne.

Wabunge wanadai kama kikomo cha umri wa miaka 75 kitaondolewa, basi Rais aliye madarakani sasa atapata mwanya wa kugombea tena mwaka 2021.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment