Friday 29 September 2017

TFF Yaanika Viingilio Mechi ya Tanzania Dhidi ya NIigeria.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka wazi viingilio vya mchezo wa marejeano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria itakayopigwa, Jumapili Oktoba mosi, mwaka huu.

Mashabiki wataingia kwenye uwanja wa Azam Complex kwa viingilio vya kawaida kushuhudia mechi hiyo timu ya taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ itakayocheza dhidi ya Falconets ya Nigeria.

Viingilio vitakuwa ni Sh. 500 tu kwa mashabiki watakaoketi eneo la mzunguko huku kwa wale watakaokaa jukwaa kuu (VIP) watalipia Sh. 1,000 tu katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam, Chamazi ulioko nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kocha wa Tanzanite, Sebastian Nkoma, amesema kwa namna alivyokiandaa kikosi chake ana imani kitaweza kupindua matokeo ya awali ambayo Tanzanite ililala mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Samuel Ogbemudian, ulioko Jimbo la Benin nchini Nigeria, wiki mbili zilizopita.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment