Sunday 17 September 2017

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Apiga Marufuku Watumishi wa Umma Kukamatwa Hovyo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepiga marufuku viongozi wa Serikali kuwakamata na kuwaweka rumande watumishi wa umma bila kufuata sheria na taratibu za utumishi.

Gambo alisema juzi kuwa siku za hivi karibuni kumejitokeza matukio ya baadhi ya viongozi kuwaweka rumande watendaji wa Serikali bila kufuata taratibu.

“Kama mtendaji alikosea kuna taratibu zake, kuna masuala ya kiutumishi, kuna ya kijinai na ya uchunguzi, hivyo ni busara kufuata taratibu,” alisema.

Gambo aliwataka viongozi kutumia vyombo vilivyowekwa na Serikali kutatua matatizo ikiwamo, Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na pia kufuata sheria za utumishi wa umma.

Pia, aliwataka watumishi wa umma mkoani Arusha kufanya kazi kwa kushirikiana na kuepuka majungu kwa kuwa wote wanawajibika kwa wananchi.

“Fanyeni kazi kwa ushirikiano na kuheshimiana ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima katika halmashauri zenu na wilaya kwa jumla,” alisema Gambo.

Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Vijijini, Wilson Mahera alisema wamejipanga kutatua kero za watumishi na wananchi ili kuhakikisha wanapata maendeleo.

Mahera alisema katika bajeti iliyopita Sh580 milioni zilitumika kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu kama kujenga nyumba za walimu, madarasa na kukabiliana na upungufu mwingine.

Alisema katika bajeti ya mwaka 2017/18 pia, mikakati imewekwa kukabiliana na kero mbalimbali za watumishi na wananchi.

Mahera alisema mapato ya ndani yanayotarajiwa kukusanywa ni zaidi ya Sh3 bilioni huku Sh39 bilioni zikitoka Serikali Kuu.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment