Saturday 20 May 2017

Aliyofunguka Meya wa Arusha Baada ya Kuachiwa Huru Leo.

Gumzo jingine la Arusha lilikua ni Meya wa Arusha, Madiwani, kiongozi wa Umoja wa wenye shule binafsi Arusha pamoja na viongozi wa dini kukamatwa na Polisi May 18 baada ya kufanya mkutano/kusanyiko kutoa rambirambi kwenye shule ya Lucy Vicent bila kibali.

Baada ya kuachiwa leo May 20 2017, Meya wa Arusha Kalist Lazaro ameongea na Waandishi wa habari na kusema >> ‘Nilikamatwa nikiwa kwenye majukumu yangu ya kawaida kabisa kama Meya wa Jiji, majukumu ya kijamii kwenye shule ya Lucky Vicent ambayo hivi karibuni ilipoteza Wanafunzi 32 kwenye ajali’

‘Tarehe 16 mimi kama Meya wa Jiji nilipewa taarifa na umoja wa shule binafsi Tanzania (TAMOSCO) na NewLIFEambayo ni NGO kutoka Ngaramtoni na baadhi ya watu wengine ambao walitaka kuhakikisha wanafikisha rambirambi zao kwa wafiwa’


‘Mimi ni Diwani wa Sokoni One, Wazazi waliofiwa wako 6 kwenye kata yangu, Diwani wa Olasiti ana familia 11 zilizofiwa… na Diwani mwingine Credo ana familia 6 zilizopoteza watoto, kwahiyo nikawaambia Madiwani wangu wahakikishe hizo familia zinakuwepo pale shuleni na mwenye shule akaandaa darasa moja ili tukio hilo lifanikiwe’

‘Moja ya vitu Wadau hao walitaka kuwe na maombi na nilimuandaa Padri waKanisa Katoliki, Mchungaji wa KKKT na kiongozi wa BAKWATA kutoka Olasiti, kabla ya zoezi la kukabidhi rambirambi mkononi kwa Wafiwa Polisi walivamia’



‘Mswali tulikua tunahojiwa ni kwanini fedha hizi hatujazipitisha kwa mkuu wa mkoa? nataka Watanzania wajue kwamba hakuna Kiongozi wa Serikali aliyefariki, walifiwa Wananchi wa kata zetu… mimi Meya wa jiji nimefiwa na Wananchi wangu’

‘Rambirambi za Wananchi zinatakiwa zipelekwe kwa waliofiwa na ndio maana siku nne zilizopita nilimtaka Mkuu wa mkoa aje hadharani awape rambirambi wale waliofiwa’ – Meya Kalist Lazaro
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment