Friday 26 May 2017

Mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg akabidhiwa shahada ya heshima.

Mwanzilishi wa Facebook na CEO Mark Zuckerberg amefanikiwa kupata shahada ya heshima kutoka katika chuo kikuu cha Havard, Marekani.

Bosi huyo ambaye ni miongoni mwa matajiri wakubwa duniani kwa mujibu wa Forbes, aliwahi kusoma katika chuo hicho miaka 12 iliyopita. Baada ya Zuck kupatiwa heshima hiyo, kupitia mtandao wake wa Facebook alimuandikia ujumbe mama yake unaosomeka, “Mom, I always told you I’d come back and get my degree.”
Miaka kadhaa iliyopita, bosi huyo aliwahi kukaririwa na gazeti la chuo hicho lijulikanalo kama “The Harvard Crimson” akisema hataweza kurudi tena chuoni hapo kusoma na badala yake atawekeza nguvu nyingi katika mtandao wake wa Facebook ambao ulikuwa unakuwa kwa kasi katika kipindi hicho.
Kwa sasa Mark mbali na kumiliki Facebook ambayo inautajiri wa $61.5 lakini pia anamiliki mitandao mingine kama Instagram na Whatsapp.Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment