Tuesday 23 May 2017

KIMENUKAA..Baada ya Makonda Kudai Nape Hakuna na Mamlaka ya Kumchunguza Katika Sakata la Clouds..Nape Amefungyka Haya Mazito.

Mbunge wa Mtama, Nape Moses Nnauye amemjia juu kwa mara nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusema kwamba hakuunda kamati ya kumchunguza yeye, bali aliunda kamati ya kuchunguza tukio la kuvamiwa kwa kituo cha utangazaji cha Clouds Media Group.
Nape ameyasema hayo mapema leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo alieleza kwamba, kama kiongozi huyo alikuwa ni mmoja wa wavamizi wa kituo hicho, basi hayupo juu ya sheria.
“Niliunda kamati kuchunguza tukio la kuvamiwa kituo cha utangazaji sio kumchunguza RC. Kama RC alikuwa mmoja wa wavamizi, hayuko juu ya sheria,” aliandika Nape
Alipoulizwa kwanini Waziri wa Habari aunde kamati ya uchunguzi wa tukio la uvamizi badala ya kamati hiyo kuundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Nape alijibu kwa kuuliza swali kama kila kamati inaundwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Majibu haya ya Nape yamekuja ikiwa ni saa chache baada ya kuulizwa ni yapi maoni yake kuhusu kauli ya Makonda kwamba hakuwa akifahamu mipaka yake ya kazi ndio sababu alikwenda kuunda tume ya kumchunguza.
Kauli ya Nape kuhusu kuunda kamati imekuja ikiwa ni takribani saa 24 tangu Makonda aliposema kuwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliunda kamati ya kumchunguza.
Makonda alisema hayo jana, ambapo alidai kuwa kamati iliyoundwa na Waziri isingeweza kumhoji kwa sababu haikuwa na uwezo huo kutokana na wajumbe wa kamati hiyo kutofahamu mambo yanayohusiana na masuala ya uvamizi.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment