Saturday 27 May 2017

Diamond Amfariji Zari Kufuatia Msiba Mzito Alioupata.

Diamond Platnumz ametuma ujumbe wa kumfariji mama watoto wake wake, Zari, kufutia msiba mzito wa Ivan ambaye ni baba watoto watatu wa Zari.

Diamond akiwa na Zari pamoja na watoto wa marehemu, Ivan. Picha hii ni yazamani

Kumekuwa na mengi yanazungumzwa kwenye mitandaoni ya kijamii kuhusu Zari, Ivan na Diamond Platnumz na mengine yamepelekea kuwakera baadhi ya mashabiki wao wa damu.

Diamond ameandika ujumbe wa kumtia moyo Zari The Boss Lady na kuonyesha yupo naye pamoja katika kipindi hicho kigumu anachopitia.


“Natamani ningekukumbatia badala ya kukutumia sms,najua upo kwenye wakati mgumu na ni mpweke, jua kwamba hauko mwenyewe, niko na wewe hapa usiku na mchana,” aliandika Diamond Instagram.

Ivan amefariki dunia Alhamisi hii nchini Afrika Kusini baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa wiki kadhaa.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment