Wednesday 31 May 2017

Imefichukaaa..Hii Hapa Sababu Kubwa Nyuma ya Pazia ka Nini Diamond Hakuhudhuria Mazishi ya Ivan Jana.

Baada ya Diamond Platnumz kutangaza kwamba angehudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga, ameshindwa kuhudhuria mazishi hayo yanayofanyika jioni hii katika makaburi ya ukoo wa marehemu yaliyoko Kayunga, nchini Uganda.
Muimbaji huyo  weekend hii alishambuliwa na mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kutokana na kitendo chake cha kufanya show nchini Kenya licha ya mama watoto wake, Zari kufiwa na mume wake huyo wa zamani.
Meneja wa msanii huyo, Sallam amedai Diamond ameshindwa kuhudhuria mazishi hayo kutokana na ratiba kuingiliana.
“Kwenye mazishi hatujahudhuria, ilikuwa twende leo alfajiri lakini sasa kumbe wao wametoka usiku kwenda kijijini. Kwa hiyo nadhani ratiba yetu imeingiliana maana na sisi tulitoka Nairobi jana jioni.” Sallam alikiambia kipindi cha U-heard cha Clouds FM.
Pia Sallam amekanusha taarifa za kwenye mitandao ya kijamii kwamba wameshindwa kuhudhuria mazishi hayo baada ya kuzuiwa airport kuingia nchini Uganga kutoka na ishu za usalama.
Alisema wao walitaka kuhudhuria mazishi hayo kwaajili ya mkupatia pole Zari  kwa kuwa huyo ndiye  mtu wao.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment