Wednesday 24 May 2017

MAHAKAMA Yatupa Ombi la Cuf Upande wa Maalim Seif la Kutaka Sakaya na Wenzake Kuzuiwa Uongozi Ndani ya Chama.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali maombi yaliyofunguliwa na Bodi ya wadhamini ya CUF dhidi ya   Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya(CUF), Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma(CUF) na wenzao sita yakuomba mahakama iwazuie kwa muda kujihusisha katika masuala ya uongozi na kufanya mikutano ya chama.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa uamuzi huo baada ya kusikiliza pande zote mbili.
Hakimu Mashauri amesema Joram Bashange ambaye aliapa katika kiapo kuwa ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini  ya CUF aliapa uongo kwa sababu bodi hiyo ilikwisha muda wake.
Hivyo, Bashange kuwa ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF ni uongo  na kwamba yeye binafsi atabeba gharama   za kesi.
Katika kesi hiyo Sakaya na wenzake walikuwa wakiwakilishwa na Wakili, Mashaka Ngole huku bodi ya wadhamini ya CUF ikiwakilishwa na Wakili Hashimu Mziray.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment