Friday 26 May 2017

Serikali kuongeza viwango vya pango la ardhi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makazi, William Lukuvi amesema kuwa Serikali itaendelea kuongeza hazina ya ardhi kwaajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwekezaji mkubwa katika sekta ya viwanda.

Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo, wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendelea ya Makazi kwa mwaka wa Fedha kwa mwaka 2017/2018 , Bungeni mjini Dodoma na kutangaza ongezeko la pango la Ardhi kwa mashamba nchini.

“Serikali inakusudia kuongeza viwango vya pango la ardhi kutoka shilingi mia 400 hadi shilingi 1000 kwa hekari kuanzia tarehe 1 mwezi wa 7 kwa mashamba ya biashara kwa mwaka yaliopimwa na kumilikishwa nje ya miji kiwango kinachotiozwa leo cha shilingi miliono 400 kwa hekari 1 ni ndogo sawa na ikilinganishwa na thamani ya pamoja na uwezo wa uzalishaji husika,” alisema Lukuvi.

“Hapa sina maana ya wakulima wadogo wadogo maskini wenye hati za kimila wale wenye hati za kimila watatozwa sifuri sifuri hawatozwi kodi yoyote.”
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment