Friday 26 May 2017

Baada ya Flora Kumkimbia...Mbasha Adai Hana Hamu na Ndoa Tena.

BAADA ya hivi karibuni aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha kuolewa na mwanaume mwingine, Mwimbaji wa Injili, Emmanuel Mbasha amefunguka kuwa hana hamu na ndoa hivyo hawezi kuwa na haraka ya kuwa na mke kwa sasa kwani anahofi a kupata mwanamke msaliti tena.

Akipiga stori na Star Mix, Mbasha alisema kutokana na changamoto kubwa aliyoipata kwenye ndoa, kila mwanamke anayemuona anamuogopa kwa kuwa ameshaumizwa kwa hiyo kwa wakati huu ameelekeza nguvu zake kwenye kazi.

“Unajua ukishaumwa na nyoka hata jani likikugusa unaogopa hivyo sina haraka ya kuoa kwa sasa, bado nipo namuomba Mungu akinionyesha nitaoa na kama haijampendeza basi nitabaki hivihivi,” alisema Mbasha.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment