Tuesday 23 May 2017

Picha ya msanii mpya wa WCB ambaye Diamond alimtambulisha.

Jana  tarahe 21, Diamond alitangaza kuwa atamtambulisha msanii mpya kutoko lebo ya Wasafi akifanya mahojiano kwa Clouds FM.
“Panapo majaaliwa siku ya jumatatu kesho, ntakuwepo kwenye LEO TENA ya Clouds fm na familia nzima ya @Wcb_wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu Mwingine Mpya toka Mtaani, ndani ya @Wcb_Wasafi….. Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umaskini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini… na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake….Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha…Siku zote naomba mkumbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond, ni ya vijana wote wapambanaji…na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti, kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo…… USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi…Shukran” Diamond aliandika  Instagram.
Hit maker huyo wa ‘Marry You’  leo kweli kamtambulisha msanii huyo mpya aitwaye Lava Lava ndani ya  kituo cha Cloud FM akiwa na Rayvanny.
Lava Lava tayari ameachia wimbo wake mpya ‘Tuachane’ akiwa Clouds FM leo. Wimbo wake pia unapatikana kwenye tovuti la Wasafi.
Huu ndo wimbo wake mpya.
https://my.notjustok.com/track/download/id/220789

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment