Thursday 25 May 2017

Ujumbe wa Diamond Platnumz Baada ya Ivan Kufariki Dunia leo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platnumz ameandika ujumbe huu "Mbele yako, Nyuma yetu" Ujumbe huo ni baada ya Aliyekuwa mume wa Zarina Hassan ‘Zari The Bosslady’, Ivan Semwanga kufariki dunia akiwa hospitali nchini Uganda alipokuwa amelazwa kutokana na matatizo ya moyo usiku wa kuamkia leo Mei 25, 2017.
Ivan aliyekuwa baba wa watoto watatu wa kiume wa Zari, aliachana na mwanamama huyo miaka michache iliyopita ambapo Zari alihamishia mapenzi kwa mwanamuziki Diamond Platinumz ambaye mpaka sasa wamezaa  watoto wawili, wa kike mmoja na wa kiume mmoja.

Ivan alikuwa maarufu Afrika Mashariki kutokana na biashara zake kubwa alizokuwa akifanya zikiwemo umiliki wa vyuo mbali mbali nchini Afrika Kusini, pamoja na Tycoon Ivan.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment