Tuesday 23 May 2017

Hatimaye mwanasheria na mshauri wa ACT wazarendo Ajiuzuru baada ya video yake chafu kuvuja.

Kutoka Mezani kwa Kiongozi wa Chama cha ACT
Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo.
Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu kutoka katika barua yake, “kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka”.
Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.
Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.
Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama – ACT Wazalendo
Dar es salaam
Mei 23, 2017.8


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment